Roger Federer amejiengua katika mshindano ya wazi ya Ufaransa mwaka huu baada ya kushindwa kupona maumivu ya mgongo yanayomkabili.
Federer mwenye miaka 34 hakuweza pia kucheza katika michuano ya wazi ya Madrid mapema mwezi huu.
Alirejea katika mashindano ya wazi ya Italia lakini aliondolewa kwenye raundi ya tatu na Dominic Thiem.
''Ninaendelea vizuri lakini sio kwa asilimia 100,''alisema mchezaji hi=uyo namba tatu kwa viwango vya mchezo huo duniani. ''Nafikiri naweza kujiweka pabaya kama nitacheza katika mashindano yoyote bila kupona vizuri''. ''Maamuzi haya hayakuwa mepesi kufanya,lakini niliamua kuacha kucheza ili pia nipumzike vyema''
Hii inamaanisha kuwa Federer atakosa kucheza Grand Slam kwa mara ya kwanza ndani ya karne hii.
Post a Comment