0
Polisi nchini Ujerumani wamewazuilia mamia ya waandamanaji wanaopinga chama cha mrengo wa kulia cha AFD.
Zaidi ya maafisa 1000 wametumwa katika eneo la mkutano wa chama hicho katika mji wa Stuttgart kutoa ulinzi.
Image copyrightJOHN MACDOUGALL AFP
Image captionKiongozi wa AFD
Polisi wametumia maji ya pilipili kuwatawanya waandamanaji waliobeba vijiti na vyuma, na kuchoma moto tairi kwenye kiingilio cha eneo la mkutano wa chama hicho, ili kuwazuia wanachama wake.
Chama hicho kinatarajiwa kuzinduliwa upya, na kutangaza wazi kuwa kinapinga dini ya kiislamu.
Image captionMaandamano dhidi ya chama cha AFD kinachopinga uislamu
Chama hicho kinapanga kupiga marufuku vazi la kidini la burqa, minara ya misikiti ambapo mwadhini hutangaza wito wa maombi, na pia kupiga marufuku mwito huo wa waadhini.

Post a Comment

 
Top