Meneja wa Manchester United Louis van Gaal anatumai kumaliza vyema msimu nchini Uingereza kwa kutwaa Kombe la FA.
United watashuka dimbani dhidi ya Crystal Palace uwanjani Wembley jioni hii.
Mechi hiyo itaanza saa moja unusu jioni saa za Afrika Mashariki.
Klabu hiyo haijashinda kombe lolote kuu tangu kuondoka kwa meneja wa muda mrefu Sir Alex Ferguson miaka mitatu iliyopita.
Van Gaal amesema kushinda fainali ya leo kutakuwa na maana kubwa zaidi kwa wachezaji wa United kushinda hata kufuzu kwa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.
Meneja wa Palace Alan Pardew kwa upande wake anataka sana kushinda kikombe hicho na asema ni muhimu sana kwake kwani atakuwa Mwingereza pili kushinda kikombe hicho katika kipindi cha miaka 21.
Fainali ya leo ni kama marudio ya fainali ya 1990.
Miaka 26 baadaye, kuna mambo mengi yaliyo sana na ya wakati huo.
Wakati huu ni meneja wa United Louis van Gaal anayekabiliwa na shinikizo lakini wakati huo ilikuwa ni meneja tofauti aliyekabiliwa na shinikizo.
Hadi pale makubwa yalipotokea.
Bao la Lee Martin katika mechi ya marudiano liliwapa United ushindi wa 1-0 na kumuwezesha Alex Ferguson kushinda kombe lake la kwanza.
Aliendelea na kabla ya kuondoka, alikuwa ameshindia klabu hiyo vikombe 38 vikuu, vitano vikiwa vya FA.
Katika kikosi cha United, wachezaji Wayne Rooney na Michael Carrick wangetaka sana kushinda, kwani hawajabahatika kushinda nishani ya FA.
Mchezaji pekee kikosi cha United aliye na nishani ya Kombe la FA ni Juan Mata aliyeshinda akiwa na Chelsea 2012.
Katika kikosi cha Palace, ni James McArthur mwenye nishani ya ushindi, baada ya kuchezea Wigan waliposhinda fainali 2013 dhidi ya Manchester City.
Post a Comment