0
Klabu ya Watford ya Uingereza imetangaza kwamba mkufunzi wa zamani wa Inter Milan Walter Mazzarri ndiye atakayekuwa meneja wao mpya kuanzia Julai.
Hii ni baada ya kuondoka kwa meneja Quique Sanchez Flores.
Mwitaliano huyo wa umri wa miaka 54, ambaye aliwahi kuwa mkufunzi Sampdoria na Napoli, ametia saini mkataba wa miaka mitatu Vicarage Road.
Mhispania Flores aliondoka baada ya kukaa chini ya mwaka mmoja Watford, ambapo aliwaongoza kumaliza nambari 13 na kufika nusufainali Kombe la FA ambapo aliondolewa na Crystal Palace.
Mazzarri ndiye meneja wa nane kupewa kazi Watford katika kipindi cha miaka minne.
Mazzarri alishinda Coppa Italia akiwa na Napoli in 2012 ana akawasaidia kumaliza nambari mbili Serie A msimu uliofuata.
Alijiunga na Inter kwa mkataba wa miaka miwili Mei 2013 na akawaongoza kumaliza nambari tano ligini msimu wake wa kwanza.
Lakini amekuwa bila kazi tangu kutimuliwa
San Siro Novemba 2014, klabu hiyo ilipokuwa nambari tisa kwenye jedwali, alama 12 nyuma ya viongozi wa ligi.

Post a Comment

 
Top