0
Wachunguzi nchini Ufaransa wamethibitisha ripoti kuwa ndege ya EgyptAir ilituma ujumbe kuwa moshi ulikuwa kwenye ndege hiyo muda mfupi kabla ianguke katika bahari ya Mediterrania.
Shirika la usalama wa safari za ndege linasema kuwa ujumbe huo unamaanisha kuanza kwa moto.
Ujumbe huo ulipokelewa muda mfupi kabla ya ndege hiyo aina ya Airbus A320 kutoweka kutoka kwa mitambo ya radar siku ya Alhamisi.
Image copyrightAFP
Image captionFamilia za waathiriwa wa ajali ya ndege.
Ndege hiyo ilikuwa safarini kutoka mjini Paris, Ufaransa na jumla ya watu 66.
Mwandishi wa BBC wa maswala ya Usalama anasema kuwa ajali hiyo huenda ikawa ni ya kawaida au ilisababishwa na mlipuko . Hata hivyo alisema uhakiki hauwezi kujulikana kwa sasa hadi chombo maalumu cha kunasa mawasiliano kwenye ndege kitakapopatikana na kuchunguzwa.

Post a Comment

 
Top