Mexico imeidhinisha kuhamishiwa Marekani mlangunzi mkuu wa madawa ya kulevya, Joaquin Guzman, almaarufu El Chapo, ili ashtakiwe kwa mauaji na ulanguzi wa madawa ya kulevya.
Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya imesema kuwa Marekani imehakikishia taifa hilo jirani kuwa Guzman hatahukumiwa kifo katika kesi zinazomkabili.
Hivi majuzi Guzman alihamishiwa gereza moja lililoko nchini Mexico hadi lingine lenye ulinzi mkali kwenye mpaka na Marekani.
Mawakili wa Guzman wamesema kuwa watakata rufaa dhidi ya uamuzi huo.
El Chapo, aliyesimamia kundi la walanguzi wa madawa ya kulevya lijulikanalo kama Sinaloa alikamatwa Januari, miezi sita baada ya kutoroka kutoka gereza moja la Ulinzi Mkali kwa kuchimba mtaro chini ya ardhi hadi katika seli yake
Post a Comment