Gavana ya jimbo Oklahoma Mary Fallin amekataa kuidhinisha mswada ambao ungeharamisha utoaji katika jimbo hilo.
Licha ya yeye mwenyewe kupinga utoaji mimba, anasema kuwa hatua hiyo haiwezi kustahimili changamoto za kisheria.
Bunge la senate la jimbo hilo liliuunga mkono mswada huo ambao unetoa fursa ya kuchukuliwa hatua za kisheria kwa madaktari ambao watasaidia kutoa mimba kwa hadi kifungo cha miaka mitatu jela.
Utoaji mimba ni halali nchini Marekani na wanaharakati wanaotetea utoaji mimba tayari wameutaja mswada huo kama ulio kinyume na sheria.
Bi Fallin amatajwa mara kadha kama mwanasiasa ambaye anaweza kuwa mgombea mwenza wa mgombea wa urais kupitia chama cha Republican Donald Trump.
Post a Comment