Wahamiaji karibu 400, wengi wao kutoka Somalia, wanahofiwa kuzama katika bahari ya Mediterranean wakijaribu kuelekea bara Ulaya.
Taarifa kutoka Misri zinasema wahamiaji hao walikuwa wakitumia boti nne kusafiri.
Jamaa za baadhi ya wahamiaji hao wamesema baadhi ya wahamiaji waliokolewa na kikosi cha wana maji kutoka Ugiriki na sasa wamo Ugiriki.
Balozi wa Somalia nchini Misri amethibitisha kisa hicho lakini akasema bado wanatafuta maelezo zaidi
Post a Comment