0

Kiongozi wa waasi nchini Sudan Kusini Riek Machar hakurejea mjini Juba leo kama ilivyotarajiwa.
Msemaji wake amesema kurejea kwa kiongozi huyo kumeahirishwa hadi kesho kwa sababu za kimipango.
Alitarajiwa kurejea leo kuchukua wadhifa mpya wa makamu wa rais wa kwanza chini ya mkataba uliofikisha kikomo mapigano ya miaka miwili nchini humo.
Dkt Machar alitoroka Juba baada ya vita kuanza Desemba 2013.
Watu zaidi ya milioni mbili wamefurushwa makwao na maelfu wengine kuuawa kwenye mapigano hayo.
Sudan Kusini ilijipatia uhuru wake kutoka kwa Sudan Julai mwaka 2011.
MacharImage copyrightReuters
Image captionMkataba wa amani ulitiwa saini Agosti mwaka jana
Dkt Machar alikuwa makamu wa rais wa Rais Salva Kiir kabla ya mapigano kuzuka.
Chini ya mkataba wa amani uliotiwa saini Agosti mwaka jana, James Wani Igga ambaye ndiye makamu wa rais wa sasa ataendelea kuhudumu katika wadhifa huo.
Dkt Machar atakuwa na mamlaka juu yake.

Post a Comment

 
Top