Mahakama nchini India imepiga marufuku mechi za kriketi katika jimbo la Maharashtra kwa sababu ya hali mbaya ya ukame katika eneo hilo.
Mahakama kuu mjini Mumbai ilitangaza kuwa mechi 13 katika ligi kuu nchini India ikiwemo fainali ambayo ilipangiwa kufanyika katika jimbo la Maharashtra mwezi ujao zifanyiwe sehemu nyingine.
Mahakama ilitupilia mbali mapendekezo kutoka kwa waandalizi kuwa watatumia maji machafu yaliyosafishwa kuandaa viwanja.
Katika sehemu zingine za jimbo hilo mabwagwa yamekauka huku hospitali zikilazimika kusitisha huduma.
Post a Comment