BAADA ya kutoka suluhu na Simba, kiungo mshambuliaji wa Azam FC, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, amefunguka licha ya usajili wa Simba kutumia mabilioni ya shilingi lakini timu hiyo imekuwa na uwezo mdogo uwanjani.
Simba inatajwa kutumia jumla ya Sh bilioni 1.3 katika usajili wake wa msimu huu na kupelekea kuwa kikosi ghali zaidi kikiwa na mastaa mbalimbali akiwemo Emmanuel Okwi, John Bocco na Haruna Niyonzima.
Sure Boy ameyasema hayo kufuatia kutoka sare ya bila kufungana na timu hiyo katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa juzi Jumamosi kwenye Uwanja wa Azam Complex ulipo Chamazi nje
kidogo la Jiji la Dar. Akizungumza Sure Boy alisema kuwa hakutarajia wapinzani wao kucheza katika kiwango cha kawaida kama ilivyotokea kwa kuwa wana timu inayodaiwa kusajiliwa kwa pesa nyingi.
“Mechi haikuwa rahisi na wala haikuwa ngumu sana ila tunashukuru kwa matokeo ambayo yametokea, tulijipanga kushinda mchezo wa leo (juzi) lakini haikuwa bahati kwa sababu ukiangalia sisi ndiyo tulikuwa bora zaidi ya wenzetu na tulistahili kushinda.
“Simba naweza kusema imecheza kwenye kiwango cha kawaida sana kwa sababu tumemiliki mpira na kufanya mashambulizi ya maana zaidi yao, ndiyo maana nasema ya kawaida kwani imekuwa tofauti na thamani yake inayosemwa,” alisema Sure Boy.
Post a Comment