0
Viongozi kutoka vyama vyote katika bunge la Marekani wamekubaliana kuhusu sheria ambayo inaruhusu vikwazo vipya kuiadhibu Urusi kwa kuingilia uchaguzi wa Marekani.
Sheria hiyo pia itapunguza uwezo wa Rais Donald Trump wa kuiondolea Urusi vikwazo.
Kipindi cha bwana Trump ofisini kimekumbwa na madai kuwa Urusi ilisaidia kushawishi uchaguzi wa mwaka uliopita.
Urusi inakana kutenda lolote baya la uchunguzi kadha ambao umefanywa na Marekania unatathmini ikiwa yeyote katika kampeni ya Trump alishirikiana na maafisa wa Urusi.
Waandishi wa habari wanasema kuwa makubaliano hayo ya Congress, yanaonyesha msimamo uliopo dhidi ya Urusi bila kujali maoni ya Trump.
Rais anaweza kuukataa mswada huo, lakini kwa kufanya hivyo inaweza kushukiwa kuwa anaiunga mkono Urusi.
Kwa upande mwingine ikiwa atautia sahihi itakuwa ni kuidhinisha sheria ambayo utawala wake unaipinga.
Mswada huo poia unaruhusu vikwazo zaidi dhidi ya Korea Kaskazini na Iran.
Sheria hiyo itaruhusu vikwazo vipya dhidi ya Urusi kwa kulimega eneo la Crimea mwaka 2014 na madai ya kuingilia uchaguzi wa Marekani.
Haki miliki ya picha EPA
Image caption Marekani ilitwaa makao ya kidiplomasia ya Urusi kwa kuingilia uchaguzi wake

Post a Comment

 
Top