Tume ya uchaguzi nchini Kenya imekubali kuruhusu vyama vya kisiasa kujiehesabi kura kwenye uchaguzi mkuu ambao utafanyika tarehe 8 mwezi Agosti mwaka huu.
Hata hivyo tume hiyo ilisema kuwa ndiyo ina ruhusa ya kutangaza matokeo ya mwisho.
Kiongozi wa upinzani Raila Odinga amezua wasi wasi mwishoni mwa wiki baada ya kuwaambia wafuasi wake kuwa muungano wa upinzani wa Nasa, utabuni kitoa chake cha kuhesabu kura na kutangaza matokeo ya uchaguzi huo.
Viongozi wa upinzani wanasema kuwa kuwepo kituo hicho itasaidia kuzuia udangayifu kwenye uchaguzi.
Rais Uhuru Kenyatta anawania uchaguzi kwenye muhula wa pili na anatarajiwa kuukabili mungano wa vyama vikuu vya upinzani.
Post a Comment