0
Raia wa Gambia wanafanya uchaguzi wao wa kwanza wa bunge hii leo tangu kiongozi wa muda mrefu Yahaya Jammeh alazimishwe kuondoka madarakani na kwenda uhamishoni.
Wakati wa utawala wake wa miaka ishirini na miwili , Rais Jammeh mara kwa mara alilipuuza bunge , na kupitisha sheria zake bila kupata ushauri wowote.
Chini ya rais mpya Adama Barrow, matarajio ni makubwa kwamba bunge la taifa litakuwa na jukumu muhimu la kutunga sheria .
Rais Adama BarrowHaki miliki ya pichaAFP
Image captionRais Adama Barrow
Baraza la mawaziri la Bwana Barrow linajumuisha wakuu wa vyama saba tofauti vya kisiasa ambao waligombea katika uchaguzi uliopita .
Chama kilichomuunga mkono Yahya Jammeh cha APRC, pia kina uwakilishi katika baraza hilo. Wagambia watatumia mfumo wa utamaduni wao wa upigaji kura wa kutupa golori ya chuma katika masanduku ya rangi moja kwa kila chama.
Wagambia watapiga kura kwa kutupa golori ya chuma katika masanduku ya rangi moja kwa kila chama.Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionWagambia watapiga kura kwa kutupa golori ya chuma katika masanduku ya rangi moja kwa kila chama.

Post a Comment

 
Top