Janga baya la njaa limetangazwa katika maeneo kadhaa nchini Sudan Kusini, likiwa ndio kali zaidi kutokea katika kipindi cha miaka sita na kuwahi kutangazwa eneo lolote duniani.
Serikali na Umoja wa Mataifa wanasema kuwa karibu watu 100,000 wanakumbwa na njaa huku wengine zaidi ya milioni moja wakiwa kwenye hataia ya kukumbwa na njaa.
Vita vya wenyewe kwa wenyewe na kuporomoka kwa uchumi vyote vimechangia kuwepo hali hiyo.
Kumetolewa onyo la kutokea njaa nchini Yemen, Somalia na Kaskazini Mashariki mwa Nigeria lakini Sudan kusini ndio ya kwanza kutangaza njaa.
Ukosefu wa chakula kwa sasa unakumba maeneo ya jimbo la Unity nchini Sudan Kusini lakini makundi ya kutoa huduma za kibinadamu yameonya kuwa hali hiyo itasanbaa kiwa hatua za dharura hazitachukuliwa.
Mashirika la kutoa misaada yakiwemo ya WFP na Unicef yanasema kuwa watu milioni 4.9 ambao ni zaidi ya asimia 40 ya watu wa Sudan Kusini wanahitaji chakula kwa dharura.
Post a Comment