0
Makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya kundi la waasi wanao ungwa mkono na Urusi na majeshi la Ukraine yanatarajiwa kufikiwa leo kwa pande mbili kusimamisha mapigano.
Uondoaji wa silaha nzito katika mstari wa mbele ni moja ya makubalino,japo kuwa hakuna ratiba kamili iliyotolewa hadi sasa.
Tangazo la kufikia hatua hiyo limetolewa mwishoni mwa wiki na waziri wamambo ya njue wa Urusi Sergei Lavrov,katika mkutano wa kimataifa wa masuala ya usalama.
Hata hivyo pia hatua hiyo ni matokeo ya mazungumzo kati ya Ukraine,Urusi,Ujerumani na Ufaransa. Na pia ni kutokana na hali ya mapigano na machafuko mashariki mwa Ukraine yaliyopamba moto mwanzoni mwa mwezi huu.

Post a Comment

 
Top