0
Mwanaume aliyebaka na kuua msichana mmoja mwaka wa 1982 amehukumiwa kifungo cha maisha jela .
Alipataikana vipi miaka 34 baadaye ?
James Warnock, 56, alimbaka na kumnyonga binti huyo mwenye umri wa miaka 17 wakati huo Yiannoulla Yianni.
Mauji hayo yaliitamausha mji wa Hampstead.
Mweka rekodi za umma za chemechembe za DNA katika mji wa London Uingereza, Nicholas Hilliard QC aliieleza jopo la majaji wa Old Bailey kuwa bi Yianni alipitia mateso ya kutisha alipokuwa mikononi mwa mshukiwa.
Yamkini Warnock alitishia kumuua binti huyo kabla ya kumbaka.
Image captionYiannoulla Yianni alikuwa na umri wa miaka 17 wakati huo
Lakini hata baada ya kukamilisha haja na tamaa yake ya mwili alimuua binti huyo aliyekuwa anaishi katika mtaa mmoja naye takriban mita mia tano kutoka makao yake.
Warnock aliendelea kuishi katika mtaa huohuo kwa sababu hakuna aliyemuona akitekeleza unyama huo, na polisi hawakuwa na sababu ya kumshuku.
Kwa miaka 34 hakuna aliyejua aliyetekeleza mauaji hayo alikuwa mmoja wao hadi majuzi tu, polisi walipomkamata akisambaza picha za utupu za watoto.
Kama ilivyoada alilazimika kutoa manii yake na mate kwa chembechembe za DNA.
Image captionJames na Yianni walikuwa wanaishi katika mtaa mmoja
Na walipofanya vipimo na kutafuta miongoni mwa kesi ambazo hazijatatuliwa, walipigwa na butwaa kupata kuwa alikuwa na chembechembe za manii sawa na ile iliyopatikana karibu na ulikopatikana mwili wa binti huyo Yiannoulla Yianni mwaka wa 1982.
Papo hapo polisi walijua kuwa ndiye aliyetekeleza mauaji hayo.
Jaji Hilliard alimhukumu akihoji kwanini binadamu ni wanyama kiasi hicho?
Kosa hilo lilipotendeka matumizi ya teknolojia ya DNA katika kuvumbua kesi mbalimbali haikuwepo na hivyo kutattua moja ya kesi za mauaji iliyobakia bila majibu kwa familia ya muathiriwa.

Post a Comment

 
Top