Vyombo vya habari nchini Syria
vinasema kuwa ndege za jeshi la Israeli, zimerusha makombora mawili
kutoka anga ya Lebanon ambayo yalianguka nje ya mji wa Damascus.
Taarifa hizo hazikusema ikiwa chochote kiliharibiwa lakini barabara kuu kutoka Lebanon kwenda Damascus hupitia mji huo.
Jeshi la Israeli halijazungumza lolote.
Ndege hizo zinaamaniwa kushambulia silaha zilizokuwa zinanuiwa kusafirishwa kwenda kwa kundi la Hezbollah nchini Lebanon.
Hezbollah ambayo ilipigana vita vilivyodumu mwezi mmoja na Israeli mwaka 2006, imetuma maelfu ya wapiganaji kumuunga mkono Rais Bashar la-Assad kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.
Mtandao wa habari wenye makao yake mjini London wa Rai al-Youm, ulinukuu taarifa zilizosema kuwa lengo la kwanza lilikuwa ghala la silaha la jeshi la Syria.
Lengo la pili ulikuwa ni msafara wa malori yaliyoaminiwa kusafirisha silaha za kundi la Hezbollah.
Post a Comment