0
Meneja wa klabu ya Arsenal ya Uingereza, Arsene Wenger ameiambia BBC kuwa hatma yake katika klabu hiyo ya Emirates inategemea jinsi matokeo ya klabu hiyo msimu huu yatakavyokuwa.
''Mkataba wangu utakamilika Juni mwakani kwa hivyo nitakachofanya baada ya hapo itategemea na matokeo ya msimu huu'' alisema Wenger.
Raia huyo wa Ufaransa 66, aliajiriwa mwezi Septemba 1996 kuiongoza klabu hiyo.
Mkataba wake wa sasa utakamilika mwishoni mwa mwezi juni mwaka ujao.
Arsenal haijashinda taji la ligi kuu ya Uingereza tangu mwaka wa 2004 jambo ambalo limechochea uhasama dhidi ya Wenger haswa kutoka kwa mashabiki wa klabu hiyo.
Awali wenger alikuwa amehusishwa na wadhfa wa kocha wa timu ya Uingereza lakini Sam Allardyce akachaguliwa kuchukua pahala pake Roy Hodgson.

Post a Comment

 
Top