Chama cha soka cha nchini England
FA, kimemfungulia mashitaka Meneja wa Manchester United Jose Mourinho
kufuatia tukio la kupiga teke chupa za maji katika mchezo wa jumapili
dhidi ya West Ham .
Taarifa ya FA imesema Mourinho alitenda kosa katika Dakika ya 27 ya mchezo uliomalizika kwa Sare ya 1-1.Kocha huyu alionyesha kuchukizwa na kitendo cha mwamuzi Jonathan Moss,kutoipa timu yake mpira wa adhabu na badala yake kumpa ya njano Kadi Paul Pogba.
Mourinho amepewa muda wa mpaka Desemba Mosi kujibu mashitaka yanayomkabili, hii ni mara ya pili kwa kocha huyu msimu huu kuingia matatani na chama cha soka cha England.
Mara ya kwanza alikwaruzana na Mwamuzi Mark Clattenburg katika mchezo dhidi ya Burnley, ambapo alifungiwa mchezo na kutozwa faini
Post a Comment