Maelfu ya Wananchi wa Cuba wameanza
kukubali matokeo kwamba rais wa zamani wa taifa hilo na
mwanamapinduzi Fidel Castro hayupo tena na hivyo kuanza kutoa heshma zao
za mwisho katika mji mkuu wa nchi hiyo Havana katika mahali
palipoandaliwa .
Mwanzo wa maombolezo ya kitaifa kulitanguliwa na
mizinga ishirini na moja ishara iliyofanywa pia katika miji ya Havana
na Santiago de Cuba, mahali ambako kiongozi huyo alitangaza mapinduzi
mnamo mwaka 1959.Waombolezaji pia walikuwa wakiweka saini za kiapo kuahidi kutekeleza uzalendo na pia kutii kanuni ya ujamaa.kuanzia Jumatano, majivu kutoka katika mwili wake utakao teketezwa yatatembezwa katika nchi hiyo kwa kupita katika vituo vyo alikofanya safari ya mapinduzi ambayo yalimuweka madarakani Fidel Castro .
Na inatarajiwa kuwa siku ya Jumapili majivu ya aliyekuwa Fidel Castro, yatazikwa katika mji wa Santiago.
Post a Comment