Huku
Yanga ikimrejesha Kocha Hans van Der Pluijm, Zesco yenyewe ikionekana
kukata tamaa kumzuia kocha wao George Lwandamina kuondoka, imempa
masharti mwalimu huyo kabla ya kumpa kibali cha kuondoka.
Lwandamina
anahusishwa na mipango ya kujiunga na Yanga kuchukua mikoba ya
Mholanzi, Pluijm ambaye hata hivyo amekataliwa kujiuzulu na klabu yake
baada ya kuchukua uamuzi huo kutokana na ujio wa Mzambia huyo wikiendi
iliyopita.
Chanzo
makini cha habari kutoka Zesco, kimesema baada ya kuona hawawezi
kumbakisha kocha huyo, wamempa masharti ya kuhakikisha anaiwezesha timu
hiyo itetee ubingwa wake wa Ligi Kuu Zambia.
"Asilimia
za Lwandamina kubaki Zesco ni ndogo sana, hivyo mara baada ya kuona
suala hilo, viongozi sasa wameamua kumwambia kocha huyo afanye kila
linalowezekana kuhakikisha klabu hiyo inatetea ubingwa wake wa ligi kuu
ili wacheze Ligi ya Mabingwa Afrika.
"Wameamua
hayo baada ya kuona kwamba Lwandamina amevutiwa zaidi na Yanga, hivyo
ili wasipoteze vitu vyote wameamua kumalizana naye kwa namna hiyo,"
kilisema chanzo hicho.
Lwandamina
aliyewahi kuinoa timu ya taifa ya Zambia 'Chipolopolo', kwa sasa
amebakisha mkataba wa miezi mitatu na Zesco ambao utaisha Januari,
mwakani.
Zesco
inashika nafasi ya nne katika Ligi ya Zambia baada ya kucheza mechi 24
na ina pointi 50, imeshinda mechi 14, imetoka sare nane na imefungwa
mara mbili. Kinara wa ligi hiyo ni Zanaco yenye pointi 65 katika mechi
28.
MECHI TANO ZA MWISHO ZESCO
Okt 12, 2016 ZESCO 2-1 Lusaka Dynamos
Okt 18, 2016 Red Arrows 1-4 ZESCO
Okt 22, 2016 Zanaco 0-0 ZESCO
Okt 26, 2016 Nkwazi 1-0 ZESCO
Leo Green Buffaloes v ZESCO
SOURCE: CHAMPIONI
Post a Comment