Watani Yanga na Simba wanakutana leo chini ya usimamizi wa Mjumbe wa Heshima wa Shirikisho la Soka Afrika (Caf), Said El Maamry.
El
Maamry anakutana na pande hizo mbili kujadili suala la beki Hassan
Kessy ambaye Simba inamlalamikia kusajili Yanga huku akijua ana mkataba
na Simba.
“Kweli
El Maamry amekubali na Jumamosi (leo), ndiyo tunakutana kwa ajili ya
kulimaliza suala hilo na Simba,” alisema mmoja wa viongozi wa Yanga
kutoka makao makuu ya Yanga, Jangwani jijini Dar es Salaam.
“Lengo
letu ni kulimaliza hili suala, kwa kuwa hii nafasi ya El Maamry ni
nzuri kwa maana hiyo ya kulimaliza, tunaamini tutafikia mwafaka.”
Kamati
ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji ambayo inashughulikia suala
hilo, ilitoa nafasi kwa Yanga na Simba kufikia mwafaka kabla yenyewe
haijatoa maamuzi.
Lakini
kama Yanga itashindwa na kuamliwa kulipa, itakuwa tatizo kwao kwa kuwa
tayari imeshamtumia Kessy katika mechi kadhaa za ligi.
Baada
ya kamati hiyo kukaa na kupata maamuzi, iliona inawezekana pia Yanga na
Simba kukutana na kulimaliza suala hilo badala ya kutoa maamuzi ambayo
yatakuwa yanauumiza upande mmoja.
Post a Comment