0
Mwanamke mmoja amejifungua watoto mapacha walioshikana nchini Syria ambapo kumeshuhudia vita vikali.
Nawras na Moaz, walizawa wakiwa wameshikana kwenye kifua na utumbo wao ukiwa nje, katika mji wa Douma mwezi Julai.
Nawras na Moaz wakipokea matibabuImage copyrightSYRIAN ARAB RED CRESCENT
Image captionNawras na Moaz wakipokea matibabu
Watoto hao wamesafirishwa kwa gari la kuwabebea wagonjwa na kupelekwa katika hospitali ya watoto karibu na mji wa Damascus.
Madaktari wa Syria wameomba msaada kutoka kwa Shirika la Afya Duniani (WHO), wakisema kwamba iwapo watoto hao hawatafanyiwa upasuaji watafariki. .
Pacha hao wamesafiri pamoja na mama yao na shangazi yao na imesemekana watoto hao wako katika hali nzuri.

Post a Comment

 
Top