Wanawake wa kiislam ndilo kundi linalonyanyaswa zaidi kiuchumi miongoni mwa makundi ya kijamii ya Uingereza, kulingana na ripoti ya wabunge.
Wana uwezekano mara tatu wa kutoajiriwa na kutafuta kazi mara mbili zaidi ya wanawake wengine huku wakiwa na uwezekano wa kutokua na shughuli yoyote ya kufanya, kulingana na Kamati ya masuala ya wanawake na usawa ya bunge.
Mawaziri lazima waanzishe mpango wa kukabiliana kutokuwepo kwa usawa kabla ya mwisho wa mwaka huu, wametoa wito wabunge.
Serikali ilisema imejitolea kuifanya Uingereza "inayomfaa kila mmoja".
"Tumepiga hatua - kwa mfano, kuna asilimia 45% ya wanawake wa kiislam kazini Zaidi ya mwaka 2011 - lakini tunafahamu kuna mengi ya kufanya ," aliongeza kusema msemaji wa serikali.
Kamati ya bunge ilisema kuwa wanawake wengi wa kiislam wanakabiliwa na "adhabu mara mbili " suala linaloathiri malengo yao ya kazi - kwa kuwa ni wanawake, wanatoka katika jamii ya walio wachache na kwa kuwa ni Waislam.
Post a Comment