0
Polisi mjini Newyork, Marekani, wanachunguza mauaji ya kasisi wa kiislamu pamoja na msaidizi wake katika eneo la Queens.
Imamu Maulama Akonjee pamoja na Tharam Uddin walipigwa risasi nyuma ya kichwa, wakati wakielekea nyumbani baada ya maombi hapo jana.
wanaume hao wawili walipigwa risasi kichwani kwa karibu na mshambulizi aliyewavizia kutoka nyuma.
Imamu Maulama Akonjee, 55, aliwasili Newyork miaka miwili iliyopita kutoka Bangladesh.
Imamu Maulama Akonjee ni mzaliwa wa BangladeshImage copyrightSHAHIN CHOWDHURY VIA AP
Image captionImamu Maulama Akonjee ni mzaliwa wa Bangladesh
Walipelekwa hospitalini japo waliaga dunia muda mfupi baadaye.
Shambulizi hilo lililotokea mchana kutwa, limeshtua jamii ya waislamu katika eneo hilo.
Baadhi ya waumini wa dini ya kiislamu wametaja shambulizi hilo kuwa la chuki dhidi ya dini ya kiislamu, na kumlaumu mwaniaji wa urais kwa tiketi ya chama cha Republican, Donald Trump, kwa kuchochea chuki dhidi ya waislamu.
"Wawili hao walikuwa wanapendwa sana. walikuwa viongozi wa jamii," Afaf Nasher, afisa wa baraza la uhusiano mwema wa Marekani na waislmu ameambia shirika la habari la Reuters. "kuna maombolezi, na kilio kikubwa cha haki."
Hata hivyo maafisa wa polisi wanasema kwamba bado hawajadhibitisha nia ama lengo la shambulizi hilo, na kwamba hawawezi kudhibitisha kwa uwazi kwamba waliuwawa kutokana na imani yao.
Malapa yalibaki kwenye eneo la mkasaImage copyrightAP
Image captionMalapa yalibaki kwenye eneo la mkasa

Post a Comment

 
Top