0
UONGOZI wa Klabu ya Stand United ya Mjini Shinyanga inayodhaminiwa na kampuni ya uchimbaji madini ya Acacia, imetangaza majina ya wachezaji 14 iliyowasajili kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu.
Wachezaji hao 14 wataungana na wachezaji wengine watakaobaki katika kikosi cha Stand United waliokuwa wakitumika msimu uliopita.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa Stand United, Alexander Sanga, tayari timu hiyo imekamilisha taratibu za usajili kwa wachezaji wake hao.
Alisema wachezaji hao wote wamesainiwa kwa mkataba wa miaka miwili kuitumikia klabu hiyo huku wawili wakitoka nje ya nchi.
Alisema lengo la usajili uliofanyika ni kuwa na kikosi imara na kuleta upinzani katika Ligi Kuu Tanzania Bara na michuano mingine.
Orodha kamili ya wachezaji hao na timu walizotoka ni; Yusuph Sabo (Coastal Union), Hassan Mpilipili (Toto Africans), Jerome Sina (Rayon Sports ya Rwanda), Wengine ni; Nurdin Mganga (Mgambo JKT), Benedictor Jacob (Lupopo fc-Congo), Hassan Salum (Coastal Union), Mussa Kirungi (Toto African), Saleh Abdallah (Kagera Sugar).
Pia wamo Jamal Mchauro (Azam Fc), Sami Ally Nuhu (JKU-Zanzibar), Fehi Abdulrahman (Mafunzo-Zanzibar), Hassan Salum (Simba SC), Zablon Anatai (Friends Rangers) na Najim Salum (Changanyikeni Fc). Pia Stand United imemsainisha mkataba mpya wa miaka miwili mshambuliaji wake nyota, Haruna Chanongo.
Kikosi cha Stand United kitaingia katika kambi rasmi itakayoanza Julai mosi jijini Dar es Salaam.

Post a Comment

 
Top