0
Mamlaka ya serikali ya Colombia imesema watu wapatao laki moja kutoka nchini Venezuela walivuka mipaka ya nchi yao mwishoni mwa wiki hii ili kwenda kununua mahitaji muhimu pamoja na dawa.
Wengi walienda safari za mbali kutoka katika miji yao nchini Venezuela kwenda kununua bidhaa muhimu ambazo zimekuwa ni ngumu mno kupatikana nchini mwao.Mipaka hiyo ilifunguliwa kwa mara ya pili mwaka huu baada ya kufungwa na rais Nicolas Maduro ambaye alisitisha uhallifu wa kuvuka mipaka.
Jumapili iliyopita watu wapatao thelathini na tano walivuka mpaka na kuelekea nchini Colombia.Upande wa upinzani wameilalamikia serikali kwa kusababisha kushuka kwa uchumi,na kusema kuwa sera zake zimetenga masuala ya biashara kuweza kuingiza malghafi na mahitaji muhimu.
Serikali hiyo imesema ,kwa sasa nchi yake inapambana na vita ya kiuchumi.

Post a Comment

 
Top