Hivi Karibuni, utakuwa huhitajiki kusafiri katika nchi za Kiafrika kwa hati nyingine kwa kuwa wewe ni Mwafrika !
Sababu kubwa hasa ni kwamba Umoja wa Afrika umezindua rasmi hati yake ya kusafiria ya kutumiwa barani!
Madhumuni ya Umoja wa Afrika kuzindua hati hiyo ili kuvunja mipaka iliyowekwa na wakoloni walipoligawanya bara la Afrika ili kulitawala karne iliyopita.
Viongozi wa bara la Afrika wamezindua hati hiyo maalum mjini Kigali, Rwanda katika kongamano la viongozi wa Afrika.
Hati zitakazotolewa kwanza zitakuwa ni za viongozi wenye hadhi ya kidiplomasia.
Wa kwanza kupewa hati hiyo ya kusafiria wamekuwa ni rais mwenyeji wa kongamano hilo Paul Kagame wa Rwanda na mwenzake wa Chad Rais Idris Deby ambaye ndiye mwenyekiti wa sasa wa AU.
Marais wote waliohudhuria kongamano hilo watapewa hati hiyo ya Umoja wa Afrika kabla ya kumalizika kwa mkutano huo.
Mawaziri wa mambo ya nchi za nje na viongozi wakuu katika umoja wa Afrika pia wanatarajiwa kujipatia hati hiyo ya kusafiria.
Umoja wa Afrika unatarajia kuwa mataifa ya Afrika yataanza kutoa hati hizo mpya za kusafiri kwa raia kufikia mwaka wa 2018.
Post a Comment