0
Ujerumani na Ufaransa zitakabiliana leo kuamua nani atakutana na Ureno katika fainali ya michuano ya ubingwa Ulaya, Euro 2016.Mechi hiyo itachezewa Stade VĂ©lodrome.
Ujerumani watakuwa bila Mats Hummels, Sami Khedira na Mario Gomez.
Bastian Schweinsteiger aliumia goti akicheza dhidi ya Italia lakini alirejea mazoezini Jumatano na ataanza dhidi ya Ufaransa, kocha Joachim Low amesema.
Kocha wa Ufaransa Didier Deschamps atalazimika kuamia iwao aendelee kumchezesha Samuel Umtiti safu ya ulinzi au amrejeshe Adil Rami, ambaye amemaliza kutumikia marufuku ya mechi moja.
Image copyrightREUTERS
Kiungo wa kati N'Golo Kante pia anarejea baada ya kutumikia marufuku.
Kikosi cha Deschamps kiko kizima na wachezaji wake wote 23 walishiriki mazoezi Jumatano.
Ufaransa hawajawahi kushinda Ujerumani katika mechi ya michuano mikubwa tangu 1958.
Alain Giresse alikuwa mchezaji wa mwisho wa Ufaransa kufunga dhidi ya Ujerumani mechi kubwa, wakati wa nusufainali ya Kombe la Dunia 1982.
Image copyrightREUTERS
Mataifa hayo mawili yalikutana mara ya mwisho Novemba 2015, mechi ya kirafiki, ambayo ilitatizwa na mashambulio ya Paris.
Ufaransa walishinda 2-0.
Ufaransa hawajafanikiwa kuondoka bila kubebeshwa goli kwenye mechi nne za karibuni zaidi katika mashindano makubwa.

Post a Comment

 
Top