Polisi nchini Italia wamemtia mbaroni mwanamme mmoja anayeshukiwa kumpiga hadi kufa mhamiaji mmoja raia wa Nigeria katika shambulizi la kibaguzi kwa misingi ya rangi.
Emmanuel Chidi amekuwa akiishi Italia tangu mwaka wa 2015, baada ya kutoroka vita nchini Nigeria.
Emmanuel Chidi alivamiwa siku ya jumanne alasiri katika mji Fermo alipokuwa akitembea na mkewe.
Ripoti zinasema raia mmoja wa Italia alimtusi mkewe Chidi matusi ya kibaguzi .
Matusi hayo yalichochea mvutano.
Mwanamme huyo raia wa Italia kwa jina Amedeo Mancini baadaye alimshambulia Chidi kwa kutumia chuma.
Chidi aliaga dunia siku moja baadaye.
Maafisa wa polisi sasa wamemkamata mwanamme huyo na kumshtaki kwa makosa ya maauji yasio ya kukusudia, yaliyochochewa na ubaguzi wa rangi.
Mauaji hayo yamelaaniwa vikali kote nchini Italia.
Waziri mkuu wa Italia bwana Matteo Renzi, amelaani vikali mauaji hayo na kusema kuwa waitaliano wote wanapaswa kupinga ubaguzi wa rangi.
Wengi wanahofia kwamba huenda ikawa ishara ya taharuki inayotokana na wahamiaji wengi wanaopewa hifadhi nchini humo kutoka barani Afrika.
Post a Comment