0
Walipuaji wa kujitoa mhanga wameshambulia sehemu takatifu kwa waislamu Wa-Shi'a nchini Iraq, katika maeneo ya kaskazini mwa mji mkuu Baghdad. Bomu moja lililipuka katika lango la kaburi la Sayid Mohammed bin Ali al-Hadi, katika mji wa Balad.
Kufuatia mlipuko huo, watu kadhaa waliokuwa na silaha, walianza kuwamiminia risasi waumini waliokuwa wakiadhimisha siku kuu ya Eid. Baadhi ya washambuliaji walijilipua. Zaidi ya watu thelathini walithibitishwa kufa.
Wakati huo huo
Wakuu nchini Saudi Arabia wamewatia mbaroni washukiwa 19 -- 12 kati yao wakiwa raia wa Pakistan -- kufuatia shambulio la bomu la kujitoa mhanga, katika msikiti wa Nabii mjini Medina, hapo siku ya Jumatatu. Msemaji wa serikali amesema kwamba, mlipuaji wa kujitoa mhanga, alikuwa na umri wa miaka 26 raia wa Saudi, ambaye alikuwa mtumiaji wa dawa za kulevya.

Post a Comment

 
Top