Kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa mataifa nchini Sudan Kusini kimesema kwamba kumekuwa na milio ya risasi zaidi katika mji wa kaskazini magharibi wa Wau.Na kwamba watu wapatao laki mbili unusu wameyahama makazi yao kwenda kwenye maeneo salama ambayo ni karibu na kambi ya vikosi vya umoja wa mataifa.
Serikali ya Sudan Imearifu kwamba wiki iliyopita watu arobaini na tatu waliaga dunia walipokuwa katika mapambano kwenye mji huo wa Wau, ingawa raia wanasema idadi ni kubwa kuliko inavyoelezwa.
Makabiliano hayo yanatoa taswira iliyodhahiri kwamba hali ya mani bado haijatengamaa Sudan Kusini,siku mbili kabla kulikuwa na maadhimisho ya miaka hamsini ya uhuru wa nchi hiyo kama taifa huru.
Wakati hayo yakijiri yameripotiwa mapigano mengine katika mji mkuu wa Juba ambapo magari ya kijeshi yalifunga barabara mashuhuda waliliambia shirika la habari la Reuters.
Post a Comment