Mahakama ya rufaa ya michezo duniani CAS imefikia makubaliano na shirikisho la riadha duniani IAAF kutatua maswala yaliyoibuka baada ya IAAF kuwapiga marufuku wanariadha wote wa Urusi kutoshiriki michezo ya Olimpiki.
Hata hivyo wanariadha 68 kutoka nchi hiyo walikwenda mahakama wakidai kauli hiyo ya IAAF inakiuka haki zao za kimsingi kwani hawajawahi kupatikana na hatia ya matumizi ya madawa ya kusisimua misuli wala kuadhibiwa na shirikisho hilo la riadha.
Kinaya ni kwamba kauli hiyo inatarajiwa kutangazwa siku 15 pekee kabla ya kufunguliwa kwa michezo hiyo ya Olimpiki.
CAS hata hivyo imeishauri IAAF kutoa tamko mapema ilikuwaruhusu wachezaji hao kujiandaa kwa mashindano.
Kamati ya Olimpiki ya Urusi hata hivyo inasisitiza kuwa mwanariadha yeyote ambaye hajathibitishwa kutumia madawa haramu hapaswi kuzuiliwa kushiriki mashindano hayo ya Rio.
CAS itatoa kauli tarehe 21 mwezi huu baada ya muafaka wa kuharakisha mambo na IAAF
Post a Comment