Mechi moja ya ligi kuu ya kandanda nchini Ecuador iliaahirishwa kwa dharura baada ya nyuki kuvamia uwanja.
Amini usiamini mechi kati ya River Ecuador na Aucas katika jiji la Guayaquil ilisimamishwa baada ya nyuki waliokuwa wakipaa kutua uwanjani.
Wachezaji kadhaa walidungwa na nyuki huku mashabiki wengi wakijeruhiwa.
Wazima moto walilazimika kuingilia kati kujaribu kuwafurusha wadudu hao.
Mechi hiyo iliyokuwa imechezwa kwa dakika kumi pekee ilisimamishwa kwa muda wa dakika 30 hivi, hata hivyo refarii katika mechi hiyo akaamua kuahirisha mechi iliyosalia.
Post a Comment