Ligi kuu ya Hispania inatarajiwa kuanza Agosti 21 kwa Mabingwa Watetezi FC Barcelona kucheza na Real Betis na Mabingwa wa Ulaya Real Madrid kuanza na Real Sociedad, Vigogo hao Wiki ijayo wanatarajiwa kurejea Mazoezini kujitayarisha na Msimu mpya.Jumatatu Barcelona watajumuika kuanza Mazoezi ya Wiki moja na kisha kwenda England kupiga Kambi kwenye Kituo cha Mazoezi cha Timu ya Taifa ya England St. George's Park.
Wakiwa huko England, Barca watacheza Mechi 3 dhidi ya Celtic, Leicester na kumalizia na Liverpool katika dimba la Wembley na kisha kurejea kwao kushiriki Kombe lao la Gamper Trophy dimba la Camp Nou na baada ya hapo wana Mechi 2 za nje na ndani kugombea taji la Supercopa dhidi ya Sevilla.
Katika maandalizi hayo Barcelona itawakosa Wachezaji kadhaa waliokuwa michuano ya ya EURO 2016 na Copa America Centenario wakiwemo wachezaji Neymar na Rafinha, ambao wataiwakilisha Brazil kwenye Michezo ya Olimpiki itakayochezwa huko huko Brazil.
Post a Comment