Mshambuliaji wa klabu ya Borussia Dortmund Henrikh Mkhitaryan amesajiliwa na klabu ya Manchester United ,kulingana na klabu hiyo ya Ujerumani.
Afisa mkuu wa Dortmund Hans-Joachim Watzke amesema kuwa wamekubali kumuuza mchezaji huyo kwa United ili kumzuia nahodha huyo wa Armenia kuwa ajenti huru mwishoni mwa msimu ujao.
''Iwapo tungekataa mchezaji huyo angekuwa huru mwaka 2017'' ,Watzke aliambia mtandao wa Dortmund.
United tayari imewasajili wachezaji wawili msimu huu akiwemo beki Eric Baily na mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic.
Mkhitayran alijiunga na Dortmund 2013 kutoka klabu ya Ukrain Shakhtar Donetsk kwa pauni milioni 23.
Post a Comment