0
KAMPUNI ya Nyumba za Watumishi (WHC) inayojenga nyumba kwa ajili ya watumishi wa umma nchini, imesema inaanza ujenzi wa awamu ya pili wa nyumba hizo, baada ya mahitaji kuwa makubwa.
Akizungumza kwenye viwanja vya Maonesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa yanayofikia tamati kesho jijini Dar es Salaam, Ofisa Uhusiano na Mauzo wa WHC, Mary Makawia, alisema katika awamu ya kwanza jumla ya nyumba 729 zilijengwa.
Nyumba hizo zilijengwa awamu ya kwanza kwenye miradi mitano iliyopo maeneo ya Kigamboni, Magomeni na Bunju, Dar es Salaam na nyingine zilijengwa Mwanza na Morogoro.
Alisema mahitaji ya nyumba kwa watumishi ni makubwa na kwamba hadi sasa wameshapokea zaidi ya maombi 1,500 ya nyumba ili hali nyumba zilizokuwepo ni 729.
Alisema kutokana na mahitaji hayo kuwa mengi, awamu ya pili ya ujenzi wa nyumba hizo utaanza kwa kujenga nyumba Dar es Salaam, Dodoma, Tanga, Pwani na Arusha na lengo lao ni kuhakikisha watumishi wote wenye kuhitaji nyumba wanapata.

Post a Comment

 
Top