0
Wanariadha kadha bingwa nchini Kenya wameshindwa kwenye mbio za kufuzu kwa michezo ya Olimpiki ambayo itafanyika mjini Rio de Janeiro mwezi Agosti.
Bingwa wa Half Marathon za Lille, Berlin na Cardiff Geoffrey Kamworor aliondoka uwanjani ikiwa imesalia mizungukuo mitatu mbio za mita 10000. Kamworor pia ndiye bingwa wa dunia wa mbio za nyika.
Mwenzake Bedan Karoki alikuwa ameondoka uwanjani akiwa amesalia na mizunguko minane.
Tanui
Image captionTanui amefuzu moja kwa moja
Mshindi wa mbio hizo alikuwa Paul Tanui aliyetumia muda wa 27:46.15 na kufuzu moja kwa moja pamoja na Charles Yosei aliyemaliza wa pili, muda wake ukiwa 27:57.07.
Kamworor na Karoki watasubiri uamuzi wa Shirika la Riadha la Kenya (AK) kufahamu iwapo watawakilisha Kenya kwenye michezo hiyo.
Upande wa wanawake, kwenye mashindano hayo yaliyofanyika uwanja wa Kipchoge Keino, mjini Eldoret magharibi mwa Kenya, Vivian Cheruiyot alishinda mbio za mita 5000 naye Helen Obiri akamaliza wa pili.
Hyvin Kiyeng alishinda mbio za mita 3000 kuruka viunzi na maji.

Post a Comment

 
Top