0
Mabingwa wa ligi nchini Uingereza Leicester wameingia katika mkataba na klabu ya CSKA Moscow kumsajili mshambuliaji wa Nigeria Ahmed Musa,kulingana na ajenti wa mchezaji huyo.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23,aliyejiunga na CSKA mwaka 2012 na kufunga mabao 54 katika mechi 168 anatarajiwa kutia saini kile ambacho BBC Sport inasema huenda ikawa kitita kikubwa zaidi kuwahi kutolewa kwa mchezaji katika klabu hiyo.
''Kila kitu kimefanikishwa na Musa atakuwa nchini Uingereza ili kufanyiwa vipimo vya kimatibabu siku ya Jumatano''.
BBC Sport ina ufahamu kwamba Musa alikataa wito wa Southampton,Everton na West Ham.
Image copyrightGETTY
Image captionAhmed Musa
Mkufunzi wa CSKA Moscow Leonid Slutsky alikiri kwamba raia huyo wa Nigeria ambaye anaweza kucheza kama winga anakaribia kuondoka katika klabu hiyo.
''Atandoka siku ya Jumanne'',Slutsky alivambia vyombo vya habari vya Urusi.

Post a Comment

 
Top