0
Andy Murray amemchapa Muastralia anayekuja juu Nick Kyrgios na kwa hivyo Andy atakutana na mfaransa Jo-Wilfried Tsonga kesho.
Wakati huo huo madada wawili ndugu Venus na Serena Williams kwa mara nyingine tena wameendelea kuonyesha kuwa umri siyo kikwazo kwa kuwa wanasalia kama kitisho katika Wimbledon.
Venus sasa ana miaka 36 na Serena ana miaka 34 lakini bado wanaendelea kuinogesha Tenisi kwa kumchapa kila wanayekutana naye hata kama ni kwa taabu.

Post a Comment

 
Top