Ni wiki mbili tu zimepita tangu mwanamuziki anayefanya vizuri nchini Marekani katika muziki wa PoP pamoja na RnB, Lady Gaga (30) kupatiwa leseni ya kwanza kwa ajili ya kuendesha gari huko California nchini Marekani.
Gaga alikuwa akiendesha gari aina ya Ford 150 SVT Lighting PickUp Truck, katika njia kuu ya Malibu huko California lakini alisimamishwa na polisi wa usalama barabarani na baadae kumshikilia kwa ajili ya maelezo Zaidi.
Mwanamama huyo aliyewahi kutamba na kibao cha “Alejandro” alijieleza kuwa hakuona kosa lake wakati akiwa barabarani kwani alikuwa akifuata sheria zote zilizowekwa barabarani na vibali vyote alikuwa ameshavikamilisha.
Maafisa wanasema kuwa Gaga hakuwa amekamilisha malipo ya Namba ya Gari hiyo (Plate Number) na alikuwa amekwishaingia barabarani ambapo ni kinyume na sheria kwani lolote linaweza kutokea kwa wakati atumiapo chombo cha usafiri.
“Kwa California, magari yote mapya na ambayo yalikwisha tumika lakini yameuzwa tena hayawezi kuwa na Leseni ya namba ya Gari, kwani hutumwa wiki zijazo mara baada ya gari kuuzwa, hivyo wamiliki wapya wa magari hayo huwa na vibali vya muda vinavyowawezesha kutumika magari hayo, lakini haikuwa hivyo kwa Lady Gaga” alisema Afisa Usalama Barabarani.
Gaga amekuwa na makosa mengi sana yatokanayo na matumizi mabaya ya barabara, kwani kwa muda mrefu amekuwa akitumia magari ya aina tofauti bila kuwa na vibali halali na wakati mwingine vibali hivyo kuisha muda wake.
Post a Comment