Mataifa mengi barani Afrika yameathirika pakubwa na baa la njaa.
Ima ni kutokana na mabadiliko ya hali ya anga , ukosefu wa pembejeo za kilimo, ama hata ukosefu wa nguvu kazi ya kuendeleza kilimo.
Kutokana na uhaba wa chakula wa mara kwa mara nchini Nigeria , Mhandisi mmoja amebuni na kuzindua trekta iliyoundwa nchini Nigeria.
Mhandisi Timothy Addigi Terfa ameiambia BBC kuwa alizindua trekta hiyo ya bei nafuu kwa sababu ya upungufu wa mashine hiyo barani Afrika na athari yake kwa kilimo nchini Nigeria.
Aidha mhandisi huyo alisema bei ya trekta barani Afrika inakohitajika mno ni ghali mno.
IJODO
Kulingana naye upungufu huo umesababisha wakulima wengi kuendelea kutumia mikono yao kuendeleza kilimo shambani na hivyo kuathiri pakubwa kiwango cha chakula kinachozalishwa.
Hilo kwa maoni yake linachangia pakubwa uhaba wa chakula nchini humo.
Kila trekta aliyounda katika karakana yake itauzwa kwa takriban dola elfu 3,500.
Trekta hizo za ''made in nigeria'' zinaitwa IJODO.
Tafsiri yake ni Kazi katika kabila la Tiv.
Post a Comment