0
Watu 9 wameuwawa katika mkanyangano, wakati wa kusherehekea sikukuu ya kiislamu ya Eid Ul-Fitr inayoadhimisha kumalizika kwa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan.
Haijabainika wazi haswa kilichosababisha mkanyangano huo katika mji wa Kumasi.
Kuna taarifa za kutatanisha ya sababu ya kukanyagana Jumatano usiku .
Vyombo vya habari nchini humo vinaripoti kwamba kulizuka vita wakati wa sherehe za maadhimisho hayo, na wakati watu walijaribu kutoroka, mkanyanganyo ukatokea.
Wengine wanasema nguvu za umeme zilipotea kwa kishindo kikubwa sawa na risasi ilofyatuliwa, na kusababisha hali ya taharuki.
Image captionHaijabainika wazi haswa kilichosababisha mkanyangano huo katika mji wa Kumasi.
Vilevile inadaiwa kuwa milango ya ukumbi huo ilikuwa imefungwa na hivyo kusababisha maafa hayo yaliyotokea.
Watu kadhaa wamejeruhiwa na wanatibiwa hospitalini.
Waliokufa ni wanawake kadhaa na wanaume watatu.

Post a Comment

 
Top