Saudi Arabia imesitisha majadiliano ya aina yoyote na jirani yake Qatar.
Tangazo
hilo la Saudia limejiri muda mfupi baada ya kinachoonekana kuwa ni
mwanya katika kuafikiana kwenye jitihada za kutatua mzozo wa kati ya
mataifa hayo mawili.Zaidi ya miezi mitatu iliyopita Saudia na mataifa mengine ya ghuba yalikatiza uhusiano na Qatar --- wakiishutumu kwa kuunga mkono makundi ya wapiganaji jihadi na kuwa karibu mno na Iran.
Lakini usiku wa kuamkia Jumamosi kiongozi wa Qatar, Sheikh Tamim na mwanamfalme wa Saudia, Mohammad bin Salman waliwasiliana kwa simu ambapo walielezea hamu yao ya kufanya mazungumzo.
Hatahivyo, muda mfupi baadaye Saudia imesitisha mazungumzo ya aina yoyote ya ziada.
Walikasirishwa na namna Qatar ilivyoripoti mawasiliano hayo ya simu --- inavyoonekana ni kwasababu vyombo vya habari havikueleza kuwa upande wa Qatar ndio ulioidhinisha mawasiliano hayo.
Post a Comment