0
Kitengo cha usalama nchini Sudan kimewaachiliwa huru wanafunzi sita wanaofanya uanaharakati waliokuwa wakizuiliwa bila mashtaka tangu msururu wa maandamano katika mji mkuu mnamo mwezi Mei, wakili wao amesema.
Maandamano hayo ghasia isababisha mamia ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Khartoum kukabiliana na vikosi vya usalama huku wakiandamana dhidi ya sera za serikali na kutaka kuwachiliwa kwa waandamanaji walioandamana.
Wanafunzi sita ambao ni wanaharakati wa kijamii wameachiliwa huru lakini wengine wanane wangali wanazuiliwa na idara ya ujasusi nchini Sudan NISS.
Vyanzo vya kibalozi ambavyo viko karibu na familia ya wanafunzi hao vimethibitisha kuwa wanafunzi hao wameachiliwa na vimesema kuwa wale walioko kizuizini huenda wakafunguliwa mashtaka.
Wakili wa wanafunzi hao amesema kuwa mazungumzo yanaendelea ili kujaribu kuhakikisha kuwa wanafunzi hao wanarejelea masomu yao katika chuo kikuu baada ya kutimuliwa na wasimamizi kufuatia maandamano hayo.
Image copyrightAP
Image captionMaandamano Sudan
Shirika la NISS lina mamlaka makubwa na katika miezi ya hivi karibuni, limewasaka wanafunzi ambao wamekuwa wakifanya maandamano na migomo katika vyuo vikuu. Aprili mwaka huu wanafunzi wawili waliuawa wakati walipokuwa wakiandamana.
Mashirika ya kutetea haki za kibinadam yameelezea wasi wasi kuhusiana na usalama wa wanafunzi hao ambao wako kizuizini.
Shirika la kimataifa la haki za kibinadam International Federation of Human Rights (FIDH) limesema kuwa limenakili visa kadhaa vya wanafunzi hao kudhulumiwa pamoja na wafungwa wengine.

Post a Comment

 
Top