0
Aliyekuwa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan, amehoji kuhusu jinsi mahakama ya kimataifa ya ICC, ilivyoshughulikia kesi zilizokuwa zikiwakumba viongozi nchini Kenya.
Gazeti la Financial Times linamnukuu Annan alihoji ikiwa Rais Uhuru Kenyatta na naubu rais William Ruto, wangebaki huru wakati wa kuendelea kwa kesi zao.
ICC ilitupilia mbali mashtaka ya uhalifu dhidi ya binadamu yaliyokuwa yakiwakumba wawili hao, lakini ikasema kuwa mashahidi walikuwa wamedhalilishwa.
Image copyrightPSCU
Image captionUhuru Kenyatta na William Ruto
Kesi hizo zilihusu ghasia zilizoshuhudiwa mwaka 2007. Watu 1500 waliuawa na wengine 600,000 kulazimishwa kuhama makwao wakati ghasa za kikabila zilisambaa kote nchini.
Kenya inasema kuwa itaondoka kutoka ICC.

Post a Comment

 
Top