Mmoja ya waimbaji maarufu nchini Pakistan Amjad Sabri amepigwa risasi na kufariki katika mji wa kusini wa Karachi.
Watu wawili waliokuwa wamejihami kwa risasi walilifyatulia risasi gari lake katika eneo la kibishara la Liakatabad polisi wamesema.
Sabri alifariki alipokuwa akipelekwa hospitalini.Haijulikani ni nani aliyepanga mauaji hayo.
Sabri alikuwa akiongoza muziki wa Sufi unaojulkana kama Qawwali.
Wasufi, ni wavumilivu, na Pakistan ina mamilioni ya wafuasi wake - lakini katika miaka ya hivi karibuni wasufi wamekuwa chini ya mashambulizi kutoka watu wenye msimamo mkali ya Kisunni.
Post a Comment