0
Polisi nchini Ujerumani wanasema kuwa muuguzi wa zamani ambaye ni mwananamme, huenda aliwaua wagonjwa wengi kwa kuwadunga sindano yenye dawa ya kutibu ugonjwa wa moyo.
Mwanamne huyo anayefahamika kama Niels H, alifungwa mwaka uliopita baada ya kuwaua watu wawili, na kwa kujaribu kuwaua wengine wawili katika mji ulio magharibi mwa nchi wa Oldenburg.
Lakini baada ya maiti 99 za wagonjwa wa zamani katika hospitali alikuwa akifanya kazi kufukuliwa, sampuli za dawa hiyo zilipatikana kwa maiti 27.
Wakati wa kesi mwaka uliopita, muuguzi huyo alisema kuwa aliwadunga wagonjwa 90 dawa hiyo kwa sababu alifurahia kuwaamsha.

Post a Comment

 
Top