KATIKA kutimiza dhamira yake ya kuwapeleka Watanzania katika ulimwengu wa sayansi na teknolojia, kampuni ya Vodacom Tanzania imezindua mfumo mpya wa kidijitali wa M-Paper.
Mfumo huo unawezesha wateja wanaotumia simu za Smartphone na kompyuta, kusoma magazeti na majarida wayapendayo kwa gharama ya nusu bei ya nakala halisi ya gazeti au jarida.
Kwa kutumia mfumo huo wa M-Paper, Vodacom imelenga kuwawezesha wateja wake, kupata taarifa zinazoandikwa kwenye magazeti na majarida wayapendao kwa urahisi kupitia simu zao za mkononi.
“Vodacom Tanzania kwa mara nyingine tumedhihirisha dhamira yetu ya kuwapeleka Watanzania katika ulimwengu wa sayansi na teknolojia kwa kuanzisha huduma hii mpya ya aina yake ya kuwawezesha kupata taarifa kupitia simu zao.
“Huduma hii pia ni mwendelezo katika kurahisisha maisha kwa wananchi, ikiwemo kubadilisha maisha ya watu kwa kupanua wigo wa ajira nchini kama ambavyo wabunifu wa programu hii wameweza kuitumia kurahisisha maisha,” alisema Rosalynn Mworia, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania.
Mworia alisema tayari magazeti na majarida zaidi ya 52, yanapatikana katika programu hiyo, ambapo wateja wanaweza kuanza kujisomea kwa gharama nafuu ya nusu bei ya nakala halisi. Pia wanaweza kuchagua namna ya kulipia kupata huduma hiyo, ambapo mteja anaweza kulipia kwa wiki kwa mwezi au kwa mwezi.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Smart Codes inayoshirikiana na Vodacom kutoa huduma hiyo, Edwin Bruno alisema wameamua kushirikiana na Vodacom, kuleta huduma hiyo ya aina yake inayowezesha Watanzania kupata taarifa kwa urahisi na kwa gharama nafuu baada ya kuona mtandao wa Vodacom, umejipanga kuhakikisha wateja wake, wanapata huduma bora kwa kutumia ubunifu wa hali ya juu wa kiteknolojia kupitia simu za mkononi.
Programu ya kusoma magazeti kwa njia ya mtandao, inapatikana katika tovuti
Post a Comment